Kijana Bonus Hyera wa kijiji cha Lusewa, akimsalimia kwa kumbusu mikono kwa shauku, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, baada ya Dk. Asha-Rose kukutana na kijana huyo, wakati wa shughuli ya uzinduzi wa tawi la CCM Kata ya Mbinga mjini, mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kijana huyo aliyeonekana kama aliyekuwa amelewa kiasi, alionyesha heshima kubwa kwa Dk. Asha-Rose, tofauti ilivyokuwa inadhaniwa na baadhi ya watu waliopomuona akimsogelea kwa shauku kiongozi huyo. |