Msomi mmoja kutoka Tanzania Aneth David Mwakilili ni miongoni mwa wasomi wengine walioteuliwa kuwania tuzo la wanasayansi wachanga barani afrika maarufu kama The Next Einstein Forum (NEF).
Aneth ni mwanafunzi wa MSc, mwaka wa mwisho, katika chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye utafiti wake wa sasa, imejikita katika kuchunguza ubora wa bacteria kwa kiingereza 'effectiveness of Bacillus strains as biocontrol, biofertilizer and biopreservative agents, and genomic comparison of the strains'.
Msomi huyu, anapenda kujikita katika uchugunzi wa maswala ya kilimo (agricultural biotechnology, agricultural bioinformatics and policies affecting translation of scientific discoveries into viable solutions).
Tuzo hiyo huleta pamoja wasomi wa sayansi, watunga sheria na washika dau katika seKta mbali mbali barani afrika, kujadili na kuhimiza sayansi inayoweza kutatua matatizo yanayokumba bara la Afrika.
Washindi wa tuzo hiyo wanapewa ufadhili na usaidizi kutoka kwa wakfu huo ili kutekeleza utafiti wao kikamilifu. Katika shindano hili Mwakilili, atafanya utafiti ambao utasaidia wakulimu kutokomeza kwekwe na hivyo kuimarisha mazao yao.