
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, kuhusiana na ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amesema Rais Kikwete anatarijiwa kuwasili leo Asubuhi ambapo pamoja na kuzindua Jengo la NSSF, Rais Kikwete pia atafungua kufungua jengo jipya la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi.
Gama amesema kuwa kazi ya tatu itakuwa ni kufungua jengo la kitega uchumi la mfuko wa Taifa ya hifadhi ya jamii, (NSSF), lililoko mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, shughuli ambazo zinatarijiwa kufanyika leo.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi hususan wakati wa uzinduzi wa jengo la NSSF ambapo pamoja na kufungua jengo hilo pia tapata fursa ya kuongea na wananchi kutokana na ukweli kwamba ujio wa Rais Kikwete ni kuunga kono juhudi za wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro katika kutekeleza miradi ya maendeleo.