Quantcast
Channel: Kijiwe chetu blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1649

KNCU YASHUSHA MTAMBO MPYA WA KUKOBOA KAHAWA KUTOKA BRAZIL.

$
0
0
Na Athumani Issa wa Kijiwe chetu Blog, Moshi

KATIKA harakati za kuboresha uzalishaji wa zao la Kahawa, Chama cha Ushirika cha Wakulima wa zao la Kahawa mkoani Kilimanjaro (KNCU), kimenunua mitambo mipya ya kukoboa Kahawa, yenye thamani ya dola laki 9.48 za kimarekani, iliyoagizwa kutoka Brazil.

Mwandishi wa mtandao wa KIJIWE CHETU BLOG alifika katika viwanja vya Kiwanda cha kukoboa Kahawa (TCCCO), kinachomilikiwa na KNCU na kushuhudia magari matano, aina ya Scania, yakipakua mitambo ya kisasa ambayo ni ya kwanza katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.

Uagizwaji wa mitambo hiyo ni moja ya maazimio ya mkutano mkuu wa KNCU kilichofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo wajumbe waliazimia kuwa  juhudi za makusudi zifanyike kunusuru kiwanda hicho.

Akizungumza na Mtandao huu, Meneja wa TCCCO, Endrew Kleruu, alisema mitambo hiyo itasaidia kupunguza upotevu wa kahawa,ikiwa ni pamoja na kuongeza ubora wa uzalishaji unaoendana na viwango vya ubora katika soko la Kimataifa.

Alisema mitambo hiyo yenye uwezo wa kuzalisha tani sita kwa saa moja itasaidia kuwapunguzia wakulima gharama za uzalishaji kutokana na uwezo wake wa kutumia umeme mdogo (30-35 KV) tofauti na mitambo wa zamani ambayo ilikuwa inazalisha tani nne tu kwa saa, ikitumia zaidi ya  100KV ya umeme.

Kwa upande wake meneja wa usambazaji vifaa wa kampuni ya Brazafric Enterprizes Ltd, Salim Mghweno, alisema kuwa ufungaji wa mitambo hiyo itatumia miezi miwili ambapo matarajio ni hadi kufikia msimu wa uzalishaji wa Kahawa mitambo huu umeshakamilika.

Mwisho.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1649

Trending Articles